Sunday, March 10, 2013

MSAFARA WA KINANA KWENDA CHINA WATUA KWA MUDA ADDIS ABABA

 Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa  Joram Mukama Biswalo (kulia) akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kushoto), baada ya kumpokea kwenye Uwanja  wa Ndege wa Kimataifa wa Adis Ababa, akitua kwa muda kwenye Uwanja huo akiwa safarini kwenda China kwa ziara ya kikazi. Wengine kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Titus Kamani. (Picha na Bashir Nkoromo).
 Msaidizi wa Katibu Mkuu wa CCM, Edward Mpogolo (kushoto) na Ofisa anayeshughulikia Siasa za Kimataifa, Makao Makuu ya CCM, Amos Siantemi wakiratibu taratibu za safari ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kwenda China, leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Maofisa hao pia walikuwa sehemu ya msafara huo.
 Mkuu wa Kitengo cha Itifaki na Uhusiano wa Kimataifa wa Makao Makuu ya CCM, D. U. H. Mshana na Mkuu wa Kitengo cha Sera za Jamii na Mahusiano ya Umma, Jasinta Mboneko  na Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM, Juliana Chitinka wauaga ujumbe wa CCM wakati ukiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliokuwa ukienda china kwenye ziara ya kikazi ya siku kumi ikiongozwa na Kinana.
 Baadhi ya viongozi na maofisa wa Chama waliopo kwenye msafara huo wakiwa kwenye basi maalum kwenda kupanda ndege ya Ehiopian Airlines wakati wa safari hiyo,
Baadhi ya viuongozi na maofisa wa Chama wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Addis Ababa baada ya msafara wa Kinana kutua kwa saa sita kwa ajili ya kuendelea na safari ya kwenda China jioni hii. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

Saturday, February 2, 2013

Dkt. Migiro atembelea Hospitali za Maweni na Ujiji Mkoani Kigoma

 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha - Rose Migiro akiwa amembeba mtoto mmoja kati ya Watoto Mapacha wa Bi. Maria Goleti Johnphas (kulia) aliejifungua mapema jana asubuhi katika Zahanati ya Ujiji,Mkoani Kigoma.Dkt. Migiro aliuongoza Ujumbe wa Umoja wa Wanawake wa Mkoa wa Kigoma kutembelea Wadi za Wazazi na Watoto katika Hospitali za Ujiji na Maweni Mkoani humo.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha - Rose Migiro akimsikiliza kwa makini mmoja wa mama alielazwa kwenye Zahanati ya Ujiji,Mkoani Kigoma.

Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha - Rose Migiro akifurahi na Mtoto aliekuwa na Mama yake nje ya Wadi ya Watoto katika Hospitali ya Maweni Mkoani Kigoma.















Friday, February 1, 2013

Dkt. Migiro azindua Mashindano ya Mpira wa Pete Mkoani Kigoma

 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro  akisalimiana na mmoja wa wachezaji wa timu ya Mwandiga Queens wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na wachezaji wa timu za Mwandiga Queens,Lake Tanganyika na Mwananchi muda mfupi kabla ya kufanyika wakwa uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro  akizungumza na wachezaji wa timu ya Shule ya Sekondari ya Mwananchi  wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akirusha mpira golini ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.

Ziara ya Dkt. Migiro Wilayani Buhigwe mkoani Kigoma

Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea maeneo hayo na kuweza kujionea changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo wananchi hao ikiwa ni pamoja na kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la Kimataifa litakalowanufaisha wakazi wengi wa wilaya hiyo ambao wako kando kando ya Mto Maragarasi unaopakana na nchi jirani ya Burundi.Dkt. Migiro pia amewaasa wananchi wa maeneo hayo kuwa na umoja,mshikamano na upendo ili kuweza kuhimarisha mambo mbali mbali ya Wilaya.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma ya asili ya kabila la Waha waliokuja kumpokea.
Wananchi wa Kijiji cha Buhigwe wakimuaga Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa CCM katika Kijiji cha Mnanila,Wilayani Buhigwe.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Mnanila kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati akiendelea na Ziara yake ya kutembelea Kata zote zilizopo wilayani humo.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwapungia watoto wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa Kijiji hicho jana.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wakimsikiliza Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro aliekuwa kwenye Ziara ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi (kulia) akikabidhi Taarifa ya Utekelezani wa Ilani ya Uchaguzi kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akipokea ripoti ya Chama Wilaya ya Buhigwe,kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Buhigwe,Bi. Bennosa Mjema.Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo,Ndg. Elisha Bagwanya
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Buhigwe wakimsikiliza Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro aliekuwa kwenye Ziara ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma ya asili ya kabila la Waha sambamba na Bibi Buchiro Edmas Kapina wakati wa Ziara ya kutembelea wilaya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akilakiwa kwa shangwe na kinamama wa Kijiji cha Kilelema.
Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Kilelema,Everist Samson akisoma taarifa ya kijiji kuhusiana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wa kijiji hizo zikiwemo zile za kuvamiwa na majambazi wanaotoka nchi jirani ya Burundi.Kijiji hiki kipo mpakani kabisa mwa Tanzania na Burundi kwa kijiji cha Buhema Mkoani Lutana,nchini Burundi.

Wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (hayupo pichani).
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilelema,Benedict Samson Mahuta (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya eneo la Soko kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati),alietembelea eneo litakalojengwa soko la Kimataifa katika Kijiji hicho cha Kilelema.
Picha ya Pamoja na Watendaji wa Kijiji cha Kilelema.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (pili kulia) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi Charles (kushoto) kuelekea kwenye eneo la mpaka wa Tanzania na Burundi unaotenganishwa na sehemu ya Mto Maragarasi.