Monday, August 6, 2012

DKT. MIGIRO AKUTANA NA WABUNGE WANAWAKE TANZANIA

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliyemaliza muda wake Dkt Asha Rose Migiro akiwa kwenye picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda pamoja na wanachama wa chama cha wabunge wanawake wa Tanzania. Dkt Migiro yupo mjini Dodoma kwa mwaliko wa Spika wa Bunge. Ametumia fursa hiyo kukutana na wabunge wanawake na kuwaasa kufanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo ya Tanzania.

Tuesday, July 31, 2012

DKT. MIGIRO AKUTANA NA JAJI WARIOBA

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba wakati Dkt. Migiro alipotembelea ofisi za Tume jijini Dar es Salaam.

Tuesday, July 24, 2012

Dkt.Asha Rose Migiro amtembelea Rais Kikwete

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na  aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa Dkt. Asha Rose Migiro ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana baada ya  kufanya mazungumzo na  aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa Dkt.Asha Rose Migiro ikulu jijini Dar es Salaam.