Monday, September 24, 2012

Dr Migiro afungua mkutano wa Serikali za mitaa Jijini Arusha

Naibu Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake,Dr Asha-Rose Migiro(wa tatu kushoto)akisalimiana na Afisa elimu Manispaa ya Arusha,Omary Mkombole mara baada ya kuwasili kufungua mkutano wa mawaziri wa serikali za mitaa wa Afrika Mashariki mjini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake,Dr Asha-Rose Migiro akifungua mkutano wa mawaziri wa serikali za mitaa wa Afrika Mashariki kwenye hoteli ya Impala mjini Arusha.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa mawaziri wa serikali za mitaa wa Afrika Mashariki kwenye hoteli ya Impala mjini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake,Dr Asha-Rose Migiro(wa nne kulia)akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja baada ya kufungua mkutano wa mawaziri wa serikali za mitaa wa Afrika Mashariki mjini Arusha.

Friday, September 21, 2012

DKT. ASHA ROSE MIGIRO MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA AMANI DUNIANI

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akimkaribisha Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Amani Duniani aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha-Rose Migiro.
Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Dr. Ishaya Nanjabu.
Dkt. Migiro akiteta jambo na Dkt. Kacou wakati Balozi wa Nigeria Dr. Nanjabu akizungumza na mmoja wa maafisa wa jeshi hapa nchini wakati wakisubiri maandamano ya Amani.
Dkt. Migiro sambamba na Dkt. Kacou wakielekea kupokea maandamano ya Wanafunzi wa Shule mbalimbali jijini Dar katika maadhimisho ya siku ya Amani Duniani.
Mgeni rasmi Dkt. Migiro (katikati), Dkt. Kacou pamoja na Balozi wa Nigeria nchini Dr. Nanjabu (kushoto) wakiwa wamebeba sanamu mfano wa ndege aina ya Njiwa ikiwa ni Ishara ya Amani.
Mgeni rasmi Dkt. Asha-Rose Migiro akiimba nyimbo za kuhamasisha Amani pamoja na washiriki wa maandamano ya siku Amani Duniani.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dkt. Alberic Kacou akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani Duniani ambapo amerejea kusisitiza kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon katika ujumbe wake wa amani mwaka huu.Amesema katika Siku ya Kimataifa ya Amani, Umoja wa Mataifa unatoa wito wa kusitishwa kabisa kwa mapigano mahali mbalimbali duniani kwa kuwa mapigano ya silaha yanashambulia mihimili muhimu ya maendeleo endelevu.Bw. Kacou pia ametumia fursa hiyo kulipongeza Bunge la Tanzania kwa dhima yake ya kuhamasisha Utawala Bora na kupiga vita ufisadi ili kuleta maendeleo ya taifa.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Amani Duniani aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani leo jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine amesema Tanzania itaendelea kuwa mfano wa jinsi demokrasi inavyofanya kazi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Aidha amesema mchakato unaoendelea wa mabadiliko ya katiba umewaweka wanaume na wanawake wa Tanzania katika nafasi ya kuamua kuhusu kuimarisha manufaa ya Kidemokrasia, kuimarisha utawala bora na haki za binadamu.
Dkt. Asha R0se Migiro akiimba pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar wakati akiondoka ukumbini hapo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dkt.Alberic Kacou akimsindikiza mgeni rasmi Dkt. Asha-Rose Migiro baada ya shereh za maadhimisho hayo.
Dkt. Asha-Rose Migiro akifanyiwa mahojiano na vyombo vya habari nchini.