Mgeni
Rasmi katika Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa
kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Wilaya ya Kinondoni,Waziri wa
Katiba na Sheria,Mh. Dkt. Asha-Rose Migiro akikata utepe kuashiria
Uzinduzi wa Mkakati huo,akishirikiana na Mbunge wa Jimbo la
Kinondoni,Mh. Iddi Azzan,Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh. Yussuf
Mwenda,Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini
(RITA),Phillip Saliboko pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni
Mhandisi Mussa Natty. Uzinduzi huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Turiani,Magomeni jijini Dar es salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),Phillip
Saliboko akitoa hotuba yake wakati wa Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na
kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Wilaya
ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo,uliofanyika leo Ukumbi wa Shule ya
Sekondari Turiani,Magomeni.
Mgeni
Rasmi katika Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa
kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Wilaya ya Kinondoni,Waziri wa
Katiba na Sheria,Mh. Dkt. Asha-Rose Migiro akitoa hotuba yake wakati wa
Uzinduzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari
Turiani,Magomeni jijini Dar es salaam.Wengine pichani toka kushoto ni
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Mh. Iddi Azzan,Meya wa Manispaa ya
Kinondoni,Mh. Yussuf Mwenda pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),Phillip Saliboko.
Sehemu
ya Wajumbe wa Elimu kutoka katika Kata mbali mbali za Wilaya ya
Kinondoni,wakifatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi kwenye Uzinduzi
wa Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule
za Msingi katika Wilaya hiyo.
Waziri
wa Katiba na Sheria,Mh. Dkt. Asha-Rose Migiro akikabidhi vyeti vya
kuzaliwa kwa baadhi ya wanafunzi kutoka Shule za msingi za Wilaya ya
Kinondoni,wakati wa Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya
kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Wilaya ya Kinondoni.
Meza kuu ikipata picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao pamoja na walimu wao.
Waziri
wa Katiba na Sheria,Mh. Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati) akimsikiliza
Msajili wa Vizazi na Vifo (RITA) Manispaa ya Kinondoni,Mariam Ling'ande
(kushoto) wakati akielezea juu ya namna RITA inavyotunza
kumbukumbu,wakati wa Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya
kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Wilaya ya Kinondoni
jijini Dar es Salaam leo.Uzinduzi huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Shule
ya Sekondari Turiani,Magomeni.