Thursday, January 31, 2013

Dkt. Asha-Rose Migiro awaasa wananchi wa Buhigwe kuwa na mshikamano

 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyangamba iliopo kwenye Kijiji cha Janda,Wilayani Buhigwe,Kigoma wakati alipoitembelea shule hiyo na kuangalia maendeleo ya Wanafunzi wa shule hiyo,alipokuwa kwenye ziara ya kukutana na wananchi wa Wilaya hiyo jana.
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwahutubia  wananchi wa Kijiji cha Muhinda kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati akiendelea na Ziara yake ya kutembelea Kata zote zilizopo wilayani humo.Dkt. Asha-Rose Migiro amewataka wananchi wa kijiji hicho kuwa na mshikamano ili kuweja kunyanyua maendeleo ya kijiji na wilaya kwa ujumla.
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa kijiji cha Viongozi mbali mbali wa CCM katika Kijiji cha Mnanila,Wilayani Buhigwe.
 Viongozi wa kijiji wakitambulishwa.

Wednesday, January 23, 2013

DK. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA BALOZI WA VIETNAM HAPA NCHINI

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kushoto) akizungumza na Balozi wa Vietnam hapa nchini,Mh. Nguyen Duy Thien, katika Ofisini Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Martine Shigela ambaye alijumuka katika mazungumzo hayo. Wengine ni Maofisa wa Makao Makuu ya CCM.
Balozi wa Vietnam hapa nchini,Mh. Nguyen Duy Thien (kushoto) akimkabidhi zawadi maalum, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.